Lowassa: "Ujumbe wa Magufuli ni kunitaka nirejee CCM, ila nilikataa"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amesema ujumbe wa Rais Magufuli kwake alipofanya nae mazungumzo Ikulu, ulikuwa ni kumshawishi arejee CCM suala ambalo hakukubaliana nalo na alimueleza Rais kwamba uamuzi wake wa kukihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA haukua wakubahatisha.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ok, kwa-hiyo na zile pongezi kwa serikali pia 'alikushawishi' uzitoe?? Hao wenzio pale ulipotoa pongezi ndipo panapowauma. Kuhusu kushawishiwa kurudi CCM ni kawaida yake JPM kusema maneno hayo......naona unajaribu 'kutuliza' hali ya hewa.......lakini zile pongezi vepe....ZIMEWACHOMA-KAMA-PASI

    ReplyDelete
  2. Usiamini kabisa huo ujumbe kuwa ni wa Lowasa kwani upo katika hali ya kutunga zaidi ili kuzima au kupunguza makali ya kauli za ukweli za pongezi juu Maghufuli na serikali yake alizozitoa muheshimiwa Lowasa. Vipi kama Maghufuli akisema hapana hakuwahi kumshawishi Lowasa kurudi CCM kitu ambacho kwa jinsi tunavyomfahamu Magufuli ni vigumu kum'bembeleza mtu . Ni kitu kisicho make any sense kwamba Magufuli alimuita Lowasa Ikulu ili amuombe arudi CCM. Na kama kweli Maghufili alitaka kumuomba Lowasa arudi CCM basi muheshimiwa raisi asingesubiri mpaka amuite Lowasa Ikulu kwani raisi ana mikono mingi na mirefu ya kumfikishia Lowasa ujumbe wake na ukamfika. Ninachokiamini mimi huwezi kuitwa kutongozwa halafu ukakubali kuingia ndani kwa mwenye kukutuongoza kama haukuwa tayari umekubali. Hayo maneno mengine ya kusema raisi kamwita Lowasa Ikulu kumuomba kurudi CCM ni upuuzi mtupu na kutaka kumpaka matope muheshimiwa kwani ikulu ni mahala pa kuzungumzia mambo ya serikali na mustakabali wa nchi. Maghufuli kama mwenye kiti wa CCM ana Office zake za chama za kuzungumzia mambo ya Chama tena nzuri tu angelimualika Lowasa kule kama alitaka kumuita kuzungumzia mambo ya chama. Kumbuka muheshimiwa Lowasa ndie aliekuwa na hamu siku nyingi ya kukatana na muheshimiwa rasi.

    ReplyDelete
  3. Sipingi hoja zako kwani hakuna anayejua ukweli zaidi ya waliokutana na kuongea...Ila Unaposema Ikulu ni mahali pa kuzungumzia mambo ya serikali inamaana unajifanya huoni mikutano ya CCM inayofanyikia Ikulu mara kwa mara au?...Mbona hiyo mikutano haendi kuifanyia kwenye hizo ofisi unazosema za chama tena nzuri?...Au Ikulu ni ofisi za Chama siku hizi?...jaribu kupunguza mihemko ya mapenzi.

    ReplyDelete
  4. Shosti, ni kweli Lowasa kamsifia JPM na JPM kamsifia Lowasa, lakini CCM hawakuumizwa na hizo sifa hata kidogo, kama ambavyo cdm zilivyowauma, ndio maana mapovu yanawatoka, ikabidi mzee wa watu alete story mpya kuwatuliza watu wake......kazi mnayo!! sera yenu cdm ukiwa mpinzani unatakiwa kupinga na kulaumu tu, NO kusifia.......hahahaha mtakufanacho-kijiba-cha-roho.......

    ReplyDelete

Top Post Ad